Lengo lake mradi huu hili hapa:
Kuongeza ulaji wa lishe ya vitamini
kwa wakazi hasa watoto.
Kutofautisha mavuno, wakulima siku
hizi wanalima mahindi na maharage tu.
Kuhakikisha mapato ya ziada kwenye
miezi kadhaa, hiyo miezi ya kipindi cha konda.
Kukusanya wakulima kwenye vikundi vya
uzalishaji ili biashara iwezeshwe.
Kukifahamisha kijiji kama eneo la
uzalishaji mwingi wa matunda na mbogamboga.
Mradi unategemea asasi ya kienyeji, FAID Friends for Agriculture Initiatives Development) inayoniajiri kama mtaalamu wa kilimo chini ya hali ya hiari. Pensheni ya kustaafu inanitosha kwa matumizi ya kila siku, kwa hiyo fedha inatumika kwenye hayo yanayofuata:
Kununua mbegu kama miti ya matunda au
mbegu za mbogamboga.
Kusafirisha hizo mbegu.
Kuajili mara kwa mara kibarua mmoja au
wawili kwenye maeneo ya mifano na kulipia gharama za utawala wa asasi.
Ufadhili utadumu miaka 3 mpaka miti iliyopandwa mwanzoni yatazaa kama miembe iliyobebeshwa au miti ya epo. Mbegu zitasambazwa kijijini Chabima ninapokaa pamoja na eneo lililopo Kusini yake Dari Salaama.
Nguvu zake mradi huu ni hizi zifuatazo kama zilizoelezwa kwenye faili la Mradi: maelezo zaidi :
Fedha kutotka ufadhili zinatumiwa kwa
ajili ya kununua miti pamoja na usafiri wake.
Mradi huu unaendeshwa na mtu
aliyeendeleza miradi mingi ya aina hii. Pengine anajua sana kiswahili na
kiingereza.
Ufuatiliaji wa mradi ni wa kiufundi na
kisayansi, pamoja na utafiti wake. Ripoti zote zinapatikana kila miezi
mitatu mtandaoni.
Mradi unaweza ukatembelewa na wale
waliochanga muda wowote.
Mradi huo uko kwenye miradi ya
maendeleo endelevu.
Mradi unajumuisha mafunzo na sio
usambazaji wa mimea tu.
Ripoti zinaonekana kwenye tovuti yawww.nyota.org tangu tarehe 1 mwezi wa 8.